Waziri Mkuu aongoza wananchi kuitazama Royal Tour
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amezitaka Halmashauri za wilaya nchini kuweka mipango ya kuibua fursa za utalii ili ziweze kunufaika na idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini baada ya hamasa kubwa iliyochochewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia filamu ya The Royal Tour.