Wahadzabe wakubali kupimiwa maeneo yao
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, ameipongeza jamii ya wawindaji ya Wahadzabe iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida kwa utayari iliyouoneha kwa kutambua na kukubali kupimiwa maeneo yao na kupatiwa hatimiliki za kimila.