
Mtaka ameyasema hayo kushukuru nafasi aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuongoza shughuli za maendeleo na kijamii katika mkoa wa Simiyu.
''Ahadi yangu kwenu na kwa watanzania ni kuwatumikia kwa vipaji vyangu vyote nilivyojaliwa na mwenyezi Mungu, namshukuru sana Mungu baba wa Mbinguni namshukuru sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa imani kubwa aliyonayo kwangu, karibuni sana Simiyu'' Amesema Mtaka
Aidha Anthon Mtaka aliteuliwa na Rais kuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu akipanda daraja kutoka mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
