Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi , amesema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva na kutokuwa na ufahamu mzuri wa njia hiyo kutokana na ugeni.
Katika ajali hiyo kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika hospitali ya Nyakahanga, na wengine katika Kituo cha afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali.



