Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Tafiti hizo zimetolewa na mashirika yanayo jishugulisha na watoto wa mitaani ya Railway Childred Africa pamoja na JUCONI utafiti uliofanyika kwa muda wa miezi 12 jijini humo na kubaini kuwa asilimia 100 ya watoto wote wa mtaani wanaambiwa maneno yasiyofaa huku asilimia 97 kati yao wa kike na wa kiume wakiwa wamedhalilishwa kijinsia na kubakwa.
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Railway Children Africa Ndugu Pete Kent amesema kuna uwezekano mkubwa watoto wa mitaani kutonufaika na mpango wa maendeleo endelevu kutokana na kutengwa na jamii hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuvunja mzunguko wa ukatili dhidi yao.
Adam Kaombwe ambaye ni mratibu wa shirika hilo amesema kutokana na hali hiyo wanaandaa Kongamano la kwanza la kimataifa la kukabiliana na ongezeko la ukatili wa watoto wanaoishi mtaani ili kuikumbusha serikali na jamii kwa ujumla kuweka ustawi na maendeleo yao na kubadilisha maisha yao.
Wakati huohuo Kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake WLAC kimeanzisha mpango wa kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia kupata huduma stahiki na kuwachukulia hatua wanaotenda ukatili huo kama ambavyo anabainisha Reema Msami ambaye ni mratibu wa Mtandao na ushawishi wa WLAC.