
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ali Idi Siwa.
Hayo yamesemwa na washiriki wa mjadala wa kisiasa uliofanyika wiki hii mjini Kigali nchini Rwanda kuhusu ukhirikiano wa kikanda.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Ofisi ya Afrika Mashariki ya Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika, ECA, Andrew Mold, chumi zote za nchi za Afrika Mashariki zimenufaika na muungano wa kibiashara wa EAC, hasa Tanzania, ambapo takwimu zinaonesha kwamba biashara yake ndani ya EAC imeongezeka mara tatu tangu mwaka 2011.
Kwa upande wake, mwalimu Thobias Knedlik, kutoka chuo kikuu cha Bremen nchini Ujerumani amesema mfano wa Muungano wa Ulaya unapaswa kuwa somo kwa ECA, kwani unanesha kwamba muungano wa kifedha umesababisha ushirikiano wa kiuchumi kuimarika zaidi.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ali Idi Siwa, amesema alichojifunza kupitia mjadala huo kuhusu ushirikiano wa kikanda barani Afrika ni kikubwa na kwamba bara la Afrika lipo katika njia ya sahihi katika kupiga hatua za maendeleo.