Patrick Mususa
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa taarifa za mwenendo wa biashara katika soko hilo kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.
Meneja Miradi na Biashara wa Soko hilo Bw. Patrick Mususa amesema katika kipindi hicho, ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umeshuka kwa asilimia 1.6 kutoka shilingi trilioni 8.3 hadi trilioni 8.2 huku idadi ya mauzo ikiwa imeongezeka kwa asilimia 73 na kufikia shilingi bilioni 3.8 kutoka mauzo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 juma moja lililopita.
Viashiria vya soko vinaonesha kuwa sekta ya viwanda wiki hii imeshuka kwa pointi 95.63 tatizo ambalo pia limeigusa sekta ya huduma za kibenki na kifedha, huku sekta ya huduma za kibiashara ikiwa imebakia kwenye kiwango kile kile kilichokuwepo wiki iliyopita.