Monday , 23rd Jan , 2017

Bibi yake na Rais wa Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, Bi, Saraha Obama ataendelea kupewa ulinzi licha ya mjukuu wake kumaliza muhula wa uongozi wake wiki iliyopita.

Obama na Bibi yake miaka kadhaa alipomtembelea nchini Kenya

 

Kwa mujibu wa gazeti la The Standard, limewakariri maafisa wa serikali ya Kenya wakisema Bi Sarah ataendelea kupatiwa ulinzi wa polisi kwa saa 24.

Makazi yake ya Kogelo katika County ya Siaya yataendelea kulindwa na watu wanaotaka kuyatembelea watalazimika kuhojiwa na kukaguliwa katika kituo cha polisi kilichopo nje ya nyumba yake.

Kabla ya kuibuka na kujulikana duniani mwaka 2006, Bi Sarah alikuwa ni mwanamke wa kawaida aliyekuwa akiuza mbogamboga katika soko la Kogelo, ambapo nyumba yake ilikuwa haina uzio wala umeme na alilazimika kutembea umbali mrefu kuchota maji.