Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bomba la mafuta mkataba waiva

Sunday , 21st May , 2017

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uganda leo wamesaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Yoweri Museveni ikulu jijini Dar es salam.

Akizungumza baada ya kutia saini tamko hilo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Museveni kwa hatua ambayo Tanzania na Uganda zimefikia katika mradi wa bomba la mafuta la Hoima – Tanga na ameeleza kuwa mradi huo ni matokeo ya urafiki na undugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

“Kwa hiyo mimi nakushukuru sana Mhe. Museveni na kwa niaba ya Watanzania wote tumefurahi sana, umetengeneza historia ya Tanzania na Uganda na pia umeimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu, Watanzania hawatakusahau” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wa Rais Museven ambaye ni mmoja wa wafuasi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika na aliyekuwa na ndoto ya kuiunganisha Afrika nzima zao ili kujipatia manufaa ya kiuchumi, ametoa wito kwa viongozi hasa vijana kuendeleza misingi ya umoja na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

"Nimefurahi sana leo, najua kuna kazi kubwa imefanyika hadi kufikia hatua hii, lakini hii pia imeonesha kuwa na sisi tunaweza” amesema Mhe. Museveni.

Tanzania na Uganda (Inter-Governmental Agreement–IGA) ambao umepangwa kukamilika katika kipindi cha wiki moja, na baada ya hapo taratibu za kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zitafanyika.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima – Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.
 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja