Monday , 14th Jan , 2019

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amedai kwamba ana wasiwasi kuwa bunge hili linalotarajiwa kuanza mapema mwezi huu halitaweza kujadili trilion 1.5 zilizoripotiwa na CAG kwamba hazionekani.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad.

Mdee amesema kuwa dalili zinaonyesha suala la kujadili taarifa za CAG halitafanikiwa kwa sababu Wajumbe wa Kamati za PAC na LAAC wamesambazwa katika Kamati zingine.

Amesisitiza kwamba imethibitishwa kuwa kamati hizo za mahesabu hazipo kwa sasa.

Mwaka 2018 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad alitoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17 ambapo alibaini sh. Trilioni 1.5 hazijulikani zilipo na zilivyotumika.

Bunge linatarajiwa kuanza tarehe 29 Januari ambapo tayarii vikao vya Kamati vimekwisha anza