Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (kulia), Prof. Abdalla Safari (katikati) pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ambaye pia alikuwa wakili upande wa utetezi Prof. Abdalla Safari akiwa ndani ya viwanja vya Mahakama Kuu na kusema hawajaridhika na hukumu hiyo kwani hakuna sababu za msingi zilizopelekea washtakiwa hao kufungwa.
Aidha, Prof. Safari amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa kukata rufaa na kuwaombea dhamana washtakiwa wao ili wakati wa kusikiliza rufaa hiyo washtakiwa wawe nje ya kifungo.
Kwa upande wake, Wakili wa Utetezi Peter Kibatala ambaye ndio anashughulikia dhamana pamoja na rufaa na kwamba ombi hilo likikubaliwa watapinga hukumu hiyo.
Kwa upande mwingine, Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli kama Mahakama ilivyosema.



