Monday , 25th Jan , 2016

Chama cha Wananchi CUF kinakutana Jumatano hii kujadili hatma ya uchaguzi Zanzibar, kubwa ikiwa ni tamko lililotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kuhusu tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo.

Mkurugezi wa Habari na Mawasiliano (CUF) Bw. Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa chama hicho kimepanga kufanya kikao maalumu cha kujadili hatma ya tangazo la Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Jussa ametoa kauli hiyo leo alipoongea na East Africa Radio kwa simu ambapo amesema mpaka sasa chama hicho hakijakubaliana na uamuzi huo wa kurudiwa kwa uchaguzi mkuu visiwani na kuamua kuitisha kikao hicho kwa majadiliano zaidi.

Amesema kuwa baadhi ya ajenda kuu ambazo wataenda kuzijadili ni pamoja na kujadili tamko lililotolewa na tume hiyo kuhusu kurudiwa uchaguzi mkuu na kutolea maamuzi ambayo watakubaliana na wanachama wao.

Hata hivyo Jussa, amewaomba wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho wanatafuta ufumbuzi wa suala hilo.