Monday , 5th Sep , 2016

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson amelishauri shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, kuangalia upya utaratibu mpya wa namna wa kupanga bajeti, na utekelezaji wake ili kupunguza mvutano katika mchakato wa kupitisha bajeti

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Dkt. Tulia amesema hayo mjini Dodoma wakati wa majumuisho ya mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya uwekezaji wa mitaji na rasimali za umma, kamati ya hesabu za serikali na kamati ya bajeti.

Dkt. Tulia ameongeza kuwa endapo mafunzo hayo yakifanyika na kwa watendaji wa serikali italeta tija zaidi katika kupitisha bajeti hiyo kwa kuwa watakuwa na uelewa sawa wa jinsi ya kuichambua bajeti.

Aidha Naibu Spika akashauri pia kamati za kisekta nazo ziweze kupewa mafunzo hayo ili zikiingia kwenye mchakato wa bajeti zijue ni nini cha kufanya kutokana na uwepo wa wabunge wapya katika bunge hilo la awamu hii.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hizo zilizopata mafunzo hayo wamesisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa itawafanya wabunge kujua ni jinsi gani bajeti ya maendeleo itakavyoenda kutekelezwa majimboni mwao.