
Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, Dkt Seif Rashid. Wizara yake ndiyo yenye jukumu la kutoa huduma kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Takwimu hizo zimetolewa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Deogratius Yinza, kwenye kikao cha wadau wa watoto waishio kwenye mazingira hatarishi na wanaoishi mitaani kwenye mkoa wa Dodoma.
Bw, Yinza ametaja sababu za watoto kukimbia nyumba zao na kuanza kuishi mitaani kuwa ni pamoja na ukatili kwa watoto, ndoa za utotoni na ndoa kuvunjika na kuwaacha watoto wakiwa hawana mahali pa kwenda.