Thursday , 5th Jun , 2014

Bajeti ya bunge la Afrika mashariki imesomwa hapo jana huku ikielezwa kuwa ni bajeti ya kuwanufaisha zaidi wana jumuiya ya Afrika mashariki.

Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki, alhaji Adam Kimbisa (kulia) akiwa na mmoja wa wawakilishi wa Tanzania katika bunge hilo Bi. Shyrose Bhanji.

Bajeti hiyo ambayo imesomwa na Naibu waziri wa wizara ya Ushirikiano wa kimataifa Abdullah Sadala kutoka nchini Tanzania amesema bajeti hiyo ya zaidi ya dola za kimarekani Mil. 124 takribani Bil. 130 za kitanzania inalenga kuboresha maisha ya wakazi wa jumuiya Afrika mashariki.

Hata hivyo baadhi ya wabunge akiwemo Shyrose Banji kutoka nchini Tanzania wamehoji
sababu za bajeti hiyo kuendelea kutegemea wafadhili kwa zaidi ya asilimia 70 katika kipindi chote cha miaka 10 ya bunge hilo na kushauri kupunguzwa kwa kiwango hicho.