Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hatma ya makontena ya Makonda

Monday , 24th Sep , 2018

Baada ya minada mitatu iliyofanyika kushindwa kupata mnunuzi wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sasa inafanya taratibu za kuyatoa bandarini ili kuyagawa bure katika taasisi za kiserikali na pamoja hospitali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa, Paul Makonda akikata utepe wakati Makontena hayo yalipowasili mwezi Februari mwaka huu.

Akizungumza na www.eatv.tv Kamishana Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema kuwa yatagawiwa bure hivi karibuni kwani sheria inaruhusu kugawa katika taasisi za kiserikali na sio binafsi pamoja na maeneo yoyote yenye huduma za kijamii, endapo mali inapokosa mteja.

Sheria inaturuhusu kugawa popote kwenye huduma za kijamii ikiwemo hospitali, kwakuwa minada yote hakuna mnunuzi aliyepatikana, kuna utaratibu ulioelekezwa kisheria wa kuziondoa mali hizo sehemu ya mnada na moja ya utaratibu huo ni kugawa bure”, amesema Kamishna Kichere.

Mara ya kwanza makontena hayo yalipigwa mnada Agosti 25, lakini yalikosa wanunuzi, watu wengi walishindwa kufikia bei iliyotakiwa, baadhi wakitaja Shilingi milioni 10 kwa kontena badala ya Shilingi milioni 60 inayotakiwa, baaada ya makontena hayo kutouzika ambapo Agosti 26, Makonda alitoa onyo akiwa mkoani Kagera kuwa atakayeyanunua atalaaniwa yeye na uzao wake. 

Agosti 27, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alikwenda bandarini kuyakagua na kuwataka viongozi wenzake serikalini kutathmini kauli zao na akawaomba wanaotaka kuyanunua wasiogope.

Akizungumza na madiwani, viongozi na watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, Agosti 30, Rais John Magufuli alizungumzia sakata hilo akiwataka viongozi kuwatumikia wananchi bila kujali wapo kwenye nafasi gani.

Umesikia hili sakata la Dar es salaam, eti Mkuu wa Mkoa ameleta makontena, ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe kodi?” Alihoji Rais Magufuli. Sheria za nchi zinasema ni mtu mmoja katika nchi mwenye dhamana ya kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya dhamana na ya misaada.

Sasa ukichukua makontena kule umezungumza na watu wengine labda na wafanyabiashara, unasema ni makontena yako halafu ukasema tena labda ni ya walimu, wala hata shule hazitajwi maana yake nini”.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba

Ziara ya Rais Samia Korea kuanza rasmi Mei 31 2024

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20