Friday , 24th May , 2024

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili wanaohusika na tukio la kumteka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 5 mwanafunzi wa shule ya awali Isaiah Samartan iliyopo jijini Mbeya.

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime akiwa mkoani Kilimanjaro amesema baada ya kuripotiwa na baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Layson Mkongwi, mfanya kazi wa kampuni binafsi huko jijini Mbeya alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika na kumweleza kuwa hatompa mtoto wake hadi atakapomtumia kiasi cha shilingi milioni ishirini.

"Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya walianza ufuatiliaji na mei 24 ,2024 majira ya saa nne usiku walifanikiwa kumkamata Winfred martin komba mwenye umri wa miaka 36 mngoni, mkazi wa vingunguti jijini Dar es salaam ambaye ndiye aliyekuwa akimpigia simu baba mzazi wa mtoto akimtisha asipotoa fedha hizo hatompa mtoto wake."

Baada ya kuhojiwa alieleza ni kweli walikula njama na mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Agness Jacob mwalubuli mkazi wa Isyesye Mbeya ili kujipatia kiasi hicho cha fedha.

"Pia alieleza baada ya kupanga njama hizo alifanikiwa kumchukua mtoto huyo mei 15 na kwenda kumficha kwa rafiki yake aitwaye Hamida Gaudience Njuu anaeishi jijini Mbeya, ufuatiliaji ulifanyika na mei 24 ,2024 majira ya saa saba kasoro usiku mtoto huyo alikutwa nyumbani kwa Hamida Gaudience njuu huko simike Mbeya."

Watuhumiwa hao ambao ni Winifred Martin Komba, Agness Jacob Mwalubuli na Hamida Gaudience Njuu wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukamilisha taratibu nyingine ili wafikishwe mahakamani.