Tuesday , 13th Dec , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Khatib M. Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Dkt. Khatib M. Kazungu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Doto James ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Khatib M. Kazungu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kutoka ikulu imesema kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.