
makontena yenye mchanga wa madini yaliyozuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam
Kamati hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni;
Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
Dkt. Oswald Joseph Mashindano
Bw. Gabriel Pascal Malata
Bw. Casmir Sumba Kyuki
Bi. Butamo Kasuka Philip
Bw. Usaje Benard Usubisye
Bw. Andrew Wilson Massawe
Wajumbe hao wataapishwa na Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hii ni kamati ya pili ya kulifuatilia suala hilo, baada ya Rais kuunda kamati nyingine wiki iliyopita, ambayo imesheni wataalam wa masuala ya madini na miamba.