Thursday , 30th May , 2019

Mwanasheria wa Baraza la Mazingira la Taifa la NEMC, Machare Heche amebainisha uwepo wa mifuko ya plastiki inayosababisha vifo vya zaidi ya viumbe hai laki moja vilivyopo baharini kutokana na mifuko hiyo kuchukua muda mrefu kuharibika.

Machale ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Afrika Break Fast cha East Radio, ikiwa ni siku 2 zimebakia kuelekea marufuku ya mifuko ya plastiki inayotarajiwa kuanza Juni Mosi 2019.

Machale amesema kuwa, "tuangalie pia faida tunayopata kama nchi, mifuko hii tunaoiondoa inaweza kukaa miaka 500, kwa hiyo kadri tunavyiong mtaani tunaharisha maisha ya watu wengine mfano sekta ya uvuvi tunahatarisha maisha mengine na sekta nyingine zaidi ya viumbe laki wanafariki sababu ya mifuko ya plastiki."

"Mikoa ambayo inategemea uvuvi ukipoteza viumbe laki moja kwa mwaka ni hasara kubwa sana, takwimu za UNEPO zinaonesha mpaka kufika 2050 tutakuwa na mifuko mingi sana kuliko samaki, yaani ukitupa nyavu yako utavua  mifuko 40 na samaki 12." ameongeza Machale Heche

Kuhusiana na gharama kuongezeka za mifuko mbadala Machale Heche amesema kuwa "Serikali kazi yetu kuweka mazingira mazuri ya atu kufanya biashara, napozungumza kuna viannda na wawekezaji zaidi ya 70, yameshaingia kwenye soko la mifuko mbadala, hiyo yote ni serikali kuhamaisha ili mifuko bei yake iweze kushuka."

Kuanzia Juni Mosi 2019, Serikali itaanza utumiaji w akanuni zinazopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.