
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
Waziri Lwenge amesema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizindua bodi ya mfumo wa maji na kuongeza kuwa miradi ya maji inayojengwa inatakiwa kulingana na thamani ya fedha wanazopatiwa kwa ajili ya ujenzi huo.
Waziri Lwenge amesema kuwa bodi hiyo ina jukumu kubwa la kupokea kubuni vyanzo mbalimbali vvya mapato na kufuatilia tathmini ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji inayoendelea na iliyoanzishwa nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba amesema sababu kubwa ya serikali kuiteua bodi hiyo ni pamoja kupata taarifa zilizo sahihi zitokanazo na bodi hiyo.