
Moja ya mabasi ambayo mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kwa kushirikiana na uongozi wa jiji la Dar es Salaam imeyapulizia dawa kuuwa mbu wanaosambaza homa hatari ya Dengue.
Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA), Halmashauri ya jiji la Dar-es-Salaam, Taboa na Polisi wamekusanyika katika kituo hicho kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa zoezi hilo.
Afisa afya wa kituo cha Ubungo, Richard Katiti, amesema kazi ya kupuliza dawa ilikuwa ya siku zote na ipo chini ya sheria ya afya ya Umma ya mwaka 2009 kifungu namba 30 ibara ya (1) ambacho kinatoa amri kwa kila mwenye chombo cha usafiri kufanya hivyo.