Wednesday , 12th Oct , 2016

Tanzania inahitaji kuendelea kuwepo kwa amani ili kuyafikia malengo ya Milenia iliyojiwekea, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa elimu unazingatiwa na kuwajengea stadi za kazi za kisasa vijana na wanafunzi.

Dkt. Jonathan Mbwambo

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia nchini Dkt. Jonathan Mbwambo alipokutana na vijana na wadau wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani lengo likiwa ni kujadili namna gani jamii ya watanzania inaweza kutekeleza malengo yake ya Milenia kwa vitendo ambavyo havivunji sheria na kukiuka haki za binadanu.

Naye Mwakilishi wa Taasisi za Dini Mchungaji Chediel Lwiza amesema kwa umoja wao viongozi wa dini watahakikisha maendeleo ya nchi yanapatika kwa njia ya amani.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Tumaini tawi la Dar es Salaam Prof. Uswege Minga amesema chuo hicho kitahakikisha kinatoa elimu ya juu ambayo itaunganisha mataifa kwa maendeleo endelevu na kuhimiza amani.