
Uamuzi huo unatokana na maombi kukiuka sheria za maombi ya marejeo ya kesi zinazoendelea katika mahakama za chini, ikiwa ni pamoja kesi hiyo inayotakiwa kuendeklea mpaka itakapo tolewa hukumu katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
Akiongea na East Africa Radio, mara baada ya hukumu hiyo, wakili wa Shekh Ponda Issa Ponda, Juma Nassoro amesema wanategemea kuchukua hatua zaidi kufuatia uamuzi huo wa mahakama kuu.
Mkurugenzi wa Mashitaka ,DPP alitoa pingamizi dhidi ya maombi ya Sheikh Ponda kusikilizwa mahakamani hapo kutokana na kukiuka Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai, kifungu kinachokataza mtu kuwasilisha maombi yoyote ya marejeo ambayo yanatokana na maamuzi au amri ya mahakama ya chini ambayo hayakumaliza kesi . kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.