
Msajili wa Hazina - Lawrence Mafuru
Uchambuzi huo pia umebaini kwamba makampuni hayo yamekabidhiwa kwa serikali kwa ajili ya maamuzi ya mwisho ikiwa ni pamoja na kutafutiwa wawekezaji wapya.
Msajili wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amesema hayo leo katika mahojiano na EATV na kufafanua kuwa idadi hiyo ni sehemu tu ya makampuni yote ambayo wamiliki wake walitakiwa kupeleka taarifa ya hali halisi ya uendelezaji wa miradi hiyo baada ya kubinafsishwa, taarifa iliyokuwa na lengo la kubaini iwapo uendelezaji unaofanywa kwenye mashirika hayo ya umma inalinufaisha taifa.
Je, ni makampuni yapi yamebainika kufanya vibaya, hapa Bw. Mafuru anataja sehemu ya mashirika na makampuni ambayo baraza la mawaziri litapitia taarifa zake na kutolea maamuzi kuwa ni pamoja na kiwanda cha nguo cha urafiki, shamba la chai la Mponde lililopo Lushoto mkoani Tanga pamoja na kiwanda cha matairi cha General Tyre.