
Dkt.Magufuli aliitangaza kamati hiyo tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma ikiongozwa na Dkt. Bashir Ally ikiwa na lengo la kuhakiki na kuchunguza mali za chama hicho.
"Nataka mali za chama zikinufaishe chama nataka mkamhoji mtu yeyote awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake.", amesema Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Bashiru Ally amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi wanaozitumia mali za chama hicho kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.