Thursday , 30th May , 2019

Mmiliki na mwanamuziki wa kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani maarufu ‘Isha Mashauzi’ amepata pigo baada ya kumpoteza mama yake mzazi, Bi Rukia Juma aliyefariki dunia jana Mei 29, 2019, ambapo anatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Mbezi kwa Msuguri. 

Bi Rukia Juma.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu na familia hiyo Said Mdoe, amsema Bi Rukia atazikwa leo saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Mbezi kwa Msuguri ambako ndio msiba ulipo. 

"Mwili utapelekwa msikitini na kutolewa baada ya ibada na kurejeshwa nyumbani tayari kwaajili ya kuelekea makaburini kwaajili ya kumpuzisha katika makazi yake ya milele", amesema Mdoe.

Bi Rukia Juma pia alikuwa mwimbaji wa taarabu katika bendi ya Mashauzi Classsic na TOT Taarab. Hili ni pigo kwa mwanamuziki Isha ambaye miaka minne iliyopita alimpoteza baba yake mzazi, Ramadhani Makongo.