
Neema Matimbe (15) akiwa na mwanaye.
Idara ya Ustawi wa Jamii ili waishi nae kwa sasa.
Imebainika kuwa mama mzazi wa Neema (15) naye ni mfanyakazi wa ndani kama alivyo mwanaye, hivyo kutokana na sababu hiyo, hospitali hiyo imesema ni vigumu kumruhusu binti huyo kwa sababu ya usalama wake.
Akizungumza na www.eatv.tv leo Januari 15, mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Ernest Ibenzi amesema mama wa binti huyo yupo lakini naye anafanya kazi za ndani jijini Dodoma, jambo ambalo ni ngumu kwa binti huyo kuruhusiwa kuishi naye.
“Changamoto ya huyu binti, Mama yake mzazi pia anafanya kazi za ndani hapa mjini, kwa hiyo hatuwezi kumruhusu kwenda huko mpaka serikali itakapopata nyumba ya kumweka baada ya kuruhusiwa, bado wapo hapa hospitalini", amesema Dkt. Ibenzi.
Mwalimu Anitha Kimako anayedaiwa kuwa mwajiri wa binti huyo ambaye anatuhumiwa kumpiga na kumshinikiza kumuweka mwanaye kabatini tangu alipozaliwa, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Januari 7 na kusomewa shtaka la kushambulia mwili ambalo alilikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Februari 7.
Wakati hayo yakiendelea, kijana anayedaiwa kumpa ujauzito binti huyo na kumkataa, Salum Waziri atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu mashtaka ya kumpa mimba mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.
Bofya link hapo chini kumsikiliza Dkt. Ibenzi.