Baadhi ya wanafunzi wanaodai kuzuiliwa matokeo yao
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wahitimu wa shule hiyo wamesema kuwa licha ya kulipa ada ya mitihani mapema wanashangazwa na uongozi wa shule kutowapatia matokeo yao kwa wakati mwafaka.
Wamesema kuwa Tangu Baraza la Mitihani Nchini (NECTA) kutangaza matokeo waliangalia kwenye mitandao mbalimbali bila kufanikiwa kuyapata hali iliyowalazimu kufika shuleni kuuliza na kuelezwa na uongozi kuwa walikuwa hawajalipa ada ya mitihani kwa wakati.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Iwambi, Mwalimu Nelusigwe Kayuni amebainisha kuwa jumla ya wanafunzi 80 wa shule hiyo wamepatiwa matokeo yao kutokana na kutimiza vigezo vya baraza na waliosalia 71 hawajapata mpaka pale watakapokamilisha ada na kwamba wamekubaliana na baadhi ya wazazi kuwa kabla ya Ijumaa ya wiki hii wawe tayari wamelipa ada.