Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mbunge CHADEMA apona kesi ya Ugaidi

Thursday , 21st Sep , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Mh.Wilfred Lwakatare  na mwenzake, Ludovick Rwezaura waliokuwa wakistakiwa kwa kosa la kula njama za kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amewaachia huru washtakiwa hao leo Alhamisi mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kisha Mahakama kuridhia.

Kishenyi ameomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu hicho kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao na  baada ya kutolewa kwa maelezo hayo hakimu aliwaachia huru washtakiwa hao leo.

Pamoja na hayo Mh. Lwakatare amemshukuru Mungu kwa kuwa na siku njema na yenye furaha.

Hata hivyo wakati kesi hiyo inaondolewa mahakamani hapo alikuwapo Mbunge Lwakatare pekee huku mshtakiwaRwezauraakiwa hajafika kwa kile kinachodaiwa kuwa na matatizo ya kifamilia.

 

Awali Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ilimfutia kesi ya makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph, baaadaye Jamhuri ilikata rufaa kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu. 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja