
Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kudaiwa kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepangwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo wakiwemo wafadhili pamoja na mbunge Lema.
Kabla ya vurugu hizo mkuu wa mkoa wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi waliokuwa wamefika kushuhudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (Maternity Africa ).
Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwemo upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo ndipo mbunge Lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndiye aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka kampuni ya Mawala Advocate na siyo kweli kwamba eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu.