
Hatua hizo za Mh. Spika zimekuja baada ya kauli zinazodhaniwa kuwa ni za Mh. Olesendeka zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge ambazo zilikuwa zikitamkwa kwa Lugha ya Kimasai, kiswahili na Kingereza.
Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari imesema kwamba , Spika ameelekeza kuwa Kamati hiyo imuite na kumhoji Kiongozi huyo ikiwa ni pamoja na kuchunguza ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.
Kauli zinazodaiwa kuwa ni za Ole- Sendeka zilisikika zikisema kwa 'bunge limemomonyolewa'.