Tuesday , 14th Aug , 2018

Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ameagiza Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza kamati ya mradi wa urasimishaji ardhi katika kata ya Kipunguni B kutokana kuwepo viashiria vya ubadhirifu wa fedha za wananchi.

Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema

Mjema ameeleza hayo leo Agosti 14, 2018 wakati alipokuwa akipokea kero kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, ambao waliokuwa wakidai kuchangishwa fedha kulipia gharama za mradi huo.

Wananchi hao walidai kuchangishwa shilingi elfu 50 kwa utambuzi na shilingi laki 4 na kamati hiyo inayojulika vinondo kwa ajili ya kupimiwa ardhi ili kusudi warasimishiwe makazi yao ikiwemo kupatiwa hati miliki.

Aidha, Mjema amesema sheria iliyoko ni kwamba wananchi wanapaswa kulipishwa shilingi laki 2.5 tu, kwa ajili huduma hiyo kutoka katika kampuni ambazo ziko kisheria.
 
"Suala hili naiagiza TAKUKURU ilifanyie kazi kwa kuifanyia uchunguzi kamati hiyo, ikibainika sheri aichukue mkondo wake, lakini utaratibu ni kwamba kampuni yeyote itapima kwa shilingi 250,000 tu si zaidi ya hiyo", amesema Mjema.
 
Mbali na hilo, Mjema amemuagiza Mkurugenzi wa wilaya kushughulikia kero za elimu hasa katika shule za kata zilizokosa uzio.

Pia ameagiza kuchukuliwa hatua kwa mwalimu wa shule ya msingi Kipunguni B, baada kumwambia  mzazi wa mmoja wa wanafunzi wazazi wao wandamane kama anaona watoto wao hawaelewi masomo.