
Kushoto ni Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na kulia ni Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Mnyika ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam eneo la Kimara Stop Over, barabara ambayo itajengwa hadi kufikia njia 8.
“Kuna hili suala la bomoabomoa tunaomba ubinadamu utumike kwa kuwalipa fidia wananchi ili kuondoa malalamiko yaliyopo,” amesema.
Mbali na suala hilo la bomoabomoa, Mnyika pia amemuomba Rais Magufuli kuondoa vikwazo vinavyoikabili demokrasia nchini.
“Demokrasia inaenda sambamba na maendeleo hivyo basi tunaomba uondoe vikwazo mbalimbali vya demokrasia,” ameongeza.
Mbali na hayo Mnyika amemuomba Rais Magufuli kutoa kauli juu ya vilio vya wananchi juu ya vyuma kukaza na kwamba hali hiyo haipo kwa mafisadi tu.
"Ukisikia Wafanyakazi wa Umma wanalilia kikokotoo, wengine wamepandishwa madaraja hawajapandishwa mishahara, Wafanyabiashara wanalia Mtaani, Rais ukipata nafasi ya kuzungumza pamoja na uzinduzi utatoa matumaini ya Taifa kwa 2019 na 2020"