Monday , 3rd Jun , 2019

Muigizaji wa filamu Bongo ambaye pia ni diwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kupitia ACT Wazalendo, Tumaini Bigilimana maarufu kama Aunt Fifi, amefariki dunia hii leo.

Taarifa juu ya kifo chake imetolewa na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, na kueleza kwamba Bi.Tumaini amefariki dunia akiwa katika hospitali ya Rabininsia iliyopo Jijini Dar es Salaam. 

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu.