
Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA, Mchungaji Petter Msigwa.
Utetezi huo wa Mchungaji Msigwa umekuja wakati akiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam kumuongezea muda wa kutosha kumtafuta Wakili mwingine wa kumtetea dhidi ya madai yanayomkabili.
Mapema juma lililopita aliyekuwa wakili wa Mchungaji Petter Msigwa, Jamhuri Johnson alitangaza kujiondoa kwenye kesi baada ya kupewa muda wa kuipitia lakini baadaye alidai kesi hiyo ilikuwa ikienda kinyume na anavyoamini.
Wakili Jamhuri Johnson anakuwa wakili wa pili kujiondoa kumsimamia Mchungaji Msigwa baada ya aliyekuwa wakili wake wa awali, Jeremiah Mtobesya kujitoa kwenye kesi hiyo august 23 mwaka huu na yeye akiwasilisha madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi hiyo.
Msigwa amesema "mawakili wangu wamekuwa wakijitoa kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Mahakama jinsi inavyoendesha kesi zake,"
"Naiomba Mahakama inipe muda wa kutosha ili niweze kutafuta wakili mzuri atakayeniwakilisha kutokana na uzito wa kesi," ameongeza Mchngaji Msigwa.
Katika shauri hilo pia leo mahakamani hapo ilishuhudia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, akiwasili mahamani baada ya kutohudhuria mara mbili baada ya kuwepo kwenye matibabu Afrika Kusini.
Viongonzi wakuu wa Chama hicho wanakabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuhamasisha uchochezi na kusababisha kifo cha aliyekuwamwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT), AkwIlina Akwilini wakati wa uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia alimshinda aliyekuwa mgombea
wa CHADEMA, Salum Mwalimu