Monday , 26th May , 2014

Jumla ya miradi 106 yenye thamani ya fedha za Tanzania Shilingi Bilioni 15.4 itatembelewa na mbio za Mwenge mkoani Mbeya mwaka huu, kati ya hiyo hamsini itazinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi na baadhi yake kukabidhiwa kwa walengwa.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akiupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili mkoani Mbeya Oktoba tatu mwaka jana.

Akizungumza katika makabidhiano ya mbio hizo katika kijiji cha Mkutano Wilayani Momba, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema katika miradi hiyo, 39 itawekewa mawe ya msingi na 17 itazinduliwa na kukabidhiwa kwa walengwa.

Miradi hiyo ni pamoja na Zahanati, Ofisi za kata, Nyumba za Waalimu pamoja na vyumba vya maabara katika shule za Sekondari.