Tuesday , 15th Aug , 2017

​Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba amejitolea kuwasomesha watoto katika kata Mgongo - Iramba mkoani Singida ambao wameshindwa kuendelea na shule kwasababu ya wazazi wao kufariki na wenye ulemavu.

Waziri Nchemba amefikia kuchukua hatua hiyo ili kuhamasisha wazazi wengine kuwapeleka shule watoto wao na kuwaondoa na mawazo ya kuwatumikisha katika ufugaji na badala yake wawatengenezee maisha bora kwa kuwapatia elimu.

Akiwa katika kata ya Mgongo Waziri Mwigulu amewakuta watoto wengi ambao wanatakiwa kuwa shule lakini hawakupelekwa kwa sababu za tamaduni za wafugaji kuwatumikisha katika ufugaji, amewataka kuwapeleka shule kwani sasa ni bure na serikali inagharamia kila kitu wao jukumu lao ni kuwaamsha tu kwenda shule.

"Jamii za wafugaji wa kisukuma na Wanyiramba muache utamaduni  wa kuwatumikisha watoto kwenye ufugaji kwani sasa hali ya maisha imebadilika sana tofauti na miaka 20 iliyopita ambapo kulikuwa na sehemu kubwa ya kufugia mifugo. Sasa mabadiliko ya hali ya hewa ni tofauti sana kwasababu ya ukame umezidi  hivyo ni wakati wa  kuwekeza katika watoto kusoma kutawasaidia baadae nyinyi wazazi"  Mh. Nchemba

Wakati huo huo ujenzi wa Hostel kila shule ya sekondari katika kata 20 unaendela kwa kasi ilikufanikisha watoto ambao wanashindwa kwenda shule kwasababu ya umbali mrefu au kuvuka mito mikubwa kuwarasishia waweze kusoma vizuri. Ujenzi huu kukamilika December mwaka huu.

Waziri Mwigulu yupo katika ziara ya kikazi jimboni kwake kukagua ilipofikia miradi ya maendeleo katika jimbo lake na ahadi alizozitoa mwaka 2015