
Awali hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili yake ili kujua kama ana matatizo ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.
Hata hivyo Nabii Tito hakuweza kufika Mahakamani siku ya leo ambapo kesi yake iliahirishwa na hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Mwajuma Lukindo baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo James Karayemaha kutokuwepo mahakamani.
Nabii Tito alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 29 mwaka 2018 na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na kiwembe kwa nia ya kuyakatisha maisha yake tukio lililotokea Januari 25 mwaka huu akiwa mahabusu.