
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Hellen Kijo-Bisima
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Hellen Kijo-Bisima wakati akitoa tamko la kituo hicho kuhusu adhabu hiyo ambayo amesema kuwa inakwenda kinyume na haki za binadamu kama inavyotafsiriwa katika matamko na mikataba mbalimbali ya Kimataifa.
Kijo-Bisimba amependekeza serikali itekeleze pendekezo la tathmini ya haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwa kuridhia mkataba wa nyongeza wa haki za kiraia na kisiasa na kutangaza rasmi sasa kuwa haitatekeleza adhabu ya kifo.
"Wakati Tanzania ikiadhimisha siku hii, ikumbukwe kuwa duniani kote adhabu ya kifo imeshafutwa katika mataifa yapatayo140 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Kimataifa la Amnesty na kati ya hizo 17 ni nchi za Kiafrika". Imesema taarifa yake.