
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani.
Akizungumza na www.eatv.tv, Katani Ahmedi Katani amedai kuwa tuhuma za yeye kutaka kuhamia CCM zilianza baada ya kuwa na ukaribu na Mbunge mwenzake wa CUF ambaye amejiuzulu na kujiunga CCM, Abdallah Mtolea siku ambayo Mbunge huyo anatangaza kujiuzulu.
Amesema kuwa “mtu hawezi kunizuia nikitaka kuhamia CCM, mimi sikuwa kwenye harakati za kutaka kuhama, kilichotokea mimi nilikuwa na Mtolea kabla ya kujiuzulu, ndiyo Mbunge Bwege akanifuata akiwa na hofu lakini nilimwambia twende bungeni nikatangaza uamuzi wa kutokuhama,”
“Kuhusu Mbatia nilimfuata juu ya kile alichozungumza na Rais Ikulu, kwa hiyo haikuwa dhambi mimi kukutana na Mbatia, na nakwambia wale ambao walitangazia kuwa nimehama nitawapeleka mahakamani kwa sababu walinivunjia utu wangu,” ameongeza.
Juzi Oktoba 20, akizungumza na www.eatv.tv, Seleman Bungara alisema “Mheshimiwa Katani aliniambia yeye ahami, lakini nilimfuata kumuuliza kuhusu kuhamia CCM akanijibu hawezi kuhama, kama kumshawishi, nilimshawishi kwa njia hiyo japo tuliongea kwa muda mrefu na nikaongea kwa muda mrefu sana kuanzia saa 7 hadi saa 11”.
“Na Kwa mujibu wa maelezo yake alivyotoka kwangu kabla ya kwenda bungeni aliniambia anaenda kwa Mbunge wa Vunjo, James Mbatia japo sikujua alizungumza nini, ila baada ya hapo alikanusha bungeni kuwa hawezi kuhama chama,” ameongeza.