Friday , 14th Oct , 2016

Afisa Mtendaji Mkuu wa mpango mpya kwa maendeleo ya Afrika, Dkt. Ibrahim Mayaki amesema nuru ya uwekezaji katika sekta ya miundombinu barani Afrika sasa inang'ara kwa kuwa mambo ya msingi yanayovutia wawekezaji yameanza kushughulikiwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mpango Mpya kwa Maendeleo ya Afrika, Dkt. Ibrahim Mayaki.

Amesema hayo jijini New York, nchini Marekani ambapo ametaja mambo hayo kuwa masuala ya kanuni za udhibiti, kuhuisha mifumo ya udhibiti, kutatua suala la vipaumbele vya miradi na kuwa na uungwaji mkono kisiasa na sasa kukamilisha suala la kupatia fedha miradi hiyo.

Bw. Mayaki ambaye anahudhuria wiki ya Afrika ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Bwawa la Sambangalou huko Afrika Magharibi la kuzalisha nishati ya umeme, bomba la kusafirisha gasi kutoka Nigeria kupitia Niger hadi Algeria na mradi wa ukanda wa kati au LAPSSET kutoka eneo la Burundi kwenda Dar es Salaam na mradi wa ukanda wa Kaskazini hadi Kusini Afrika.

Amesema mpango wa NEPAD wa uendelezaji wa miundombinu Afrika, PIDA umerahisisha uwekezaji na kwamba miradi hiyo imewezekana baada ya Kuweza kuwashawishi wawekezaji kwa msingi wa mifano halisi.

Lakini kwa misingi ya utawala bora katika nchi ambako tunaenda kuwekeza kumewezesha wapate faida ambayo wasingaliweza kupata katika nchi nyingine duniani.