
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam Mkurugenzi Mawasiliano Nyumba za Watumishi wa Umma nchini, Maryjane Makawia amesema kuwa serikali imeliona tatizo hilo la uhaba wa nyumba za watumisha wa umma na zisizo na ubora, hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo bado miundombinu yake haijaimarika,hivyo wameamua kuingia mikataba na mabenki mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea watumishi hao nyumba ambazo watazimudu kulingana na vipato vyao.
Amesema katika kuboresha ufanisi wa wafanyakazi nchini niwajibu wa serikali kuboresha makazi ya watumishi hao ikiwa ni njia moja wapo yakuwapa motisha wa kufanya kazi kwani taifa likiwa na makazi bora kwa wafanyakazi wake taifa litazalisha wataalamu wa kada mbalimbali kwa wingi zaidi.
