Friday , 6th Jun , 2014

Jeshi la polisi nchini Tanzania limezindua kampeni ya kuzuia uhalifu iliyopewa jina la “sote kwa pamoja tunaweza kukataa uhalifu” ili kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaohusisha wahalifu kutoka nchi zaidi ya moja.

Naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania, Abdulrahman Kaniki.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai DCI Isaya Mngulu amesema jeshi la polisi limeweka mikakati ya kuendelea kudhibiti nchini Tanzania.

Kwa upande wake Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahman Kaniki, amesema kampeni hiyo ni mahsusi na yenye lengo la kuhimiza na kuelemisha jamii madhara ambayo husababishwa na vikundi vya kihalifu.