Thursday , 24th Mar , 2016

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein amesema anawapongeza viongozi wote na wagombea wengine 13 ambao walishiriki uchaguzi kwa kukubali matokeo ya uchaguzi.

Rais Dkt. Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya kwanza kama Rais baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omari Othman Makungu mbele ya viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa taasisi binafsi pamoja na mamia ya wananchi katika uwanja wa Amani Zanzibar.

''Nawapongeza wagombea wenzangu kwa kukubali matokeo kwa maelezo yao ya pamoja yaliyosomwa na Hamad Rashid kwa upande wangu nawaahidi nitashirikiana nao katika kuiletea maendeleo ya Zanzibar''-Amesema Dkt.Shein

Aidha Rais Dkt. Shein amesema Serikali atakayoiunda atahakikisha inashirikiana na upande wa Bara katika kuwaletea maendeleo wananchi.