Thursday , 16th May , 2019

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri mbili, ambazo ni Mbozi mkoani Songwe pamoja na Uyui mkoani Tabora kuanzia leo Mei 16, 2019.

Rais John Magufuli

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Rais amewatumbua Bw. Adelius Kazimbaya Makwega wa Mbozi na Bi. Hadja Makuwani wa Uyui Tabora.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa wakurugenzi wapya kwenye halmashauri hizo utafanyika baadaye.