Thursday , 24th Mar , 2016

Mchango wa kiuchumi utokanao na rasilimali za misitu nchini bado ni mdogo kutokana na kutokwepo kwa miongozo rahisi ya matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.

Mjumbe wa Kampeni ya Mama Misitu ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu nchini SHIVIMITA, Bw. Ben Mfungo Sulus,

Mjumbe wa Kampeni ya Mama Misitu ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu nchini SHIVIMITA, Bw. Ben Mfungo Sulus, amesema hayo jana wakati utoaji wa taarifa ya mafanikio ya Kampeni ya Mama Misitu na jinsi ilivyoweza kuchochea utunzaji na matumizi bora ya misitu..

Bw. Sulus amesema waatanda mfumo ambao utawawezesha jinsi gani Watanzania waishio maeneo ya vijijini wanavyoweza kutunza misitu katika njia ambazo ni sahihi na zinazoweza kuboresha hali zao za kiuchumi.

Meneja Kampeni hiyo Bw. Gwamaka Mwakanjala amesema moja ya mafanikio ya kampeni hiyo ni kutolewa kwa miongozi sahihi ya matumizi bora na endelevu ya misitu na jinsi wananchi wanavyoweza kutumia miongozi hiyo kunufaika kiuchumi...

Kwa upande wake, Mratibu wa Kikundi Kazi cha Misitu Bw. Cassian Sianga amesema kabla ya kutolewa miongozi hiyo wananchi walikuwa hawana ufahamu wa ukubwa wa rasilimali za misitu waliyonayo na kwamba kama wadau wa misitu iliwabidi kufanya tafsiri ya sheria ya misitu ili kuja na machapisho yanayoonyesha umuhimu wa misitu kwa wananchi