Akiongea leo jijini Dar es salaam, Dkt. Posi amesema watu wanaotumia maandishi ya nukta nundu wananyimwa haki ya kupata habari kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria inataka vituo vya televisheni kuweka wakalimani wa lugha ya alama katika habari za kitaifa.
Dkt. Posi amesema suala la ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya habari ni mdogo ikiwa ni pamoja na kuwapa ajira watu wenye albinism kuwa watangazaji wa vipindi vingine tofauti na ilivyozoeleka walemavu kufanya vipindi vinavyowahusu pekee.