Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa kutokana na vurugu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2007-2008 ambapo watu 1200 walipoteza maisha huku wengi wakibakia vilema na kupoteza mali zao na kuwa wakimbizi ndani ya nchi hiyo.
Mashahidi sita waliokuwa wanamhusisha Bwn Ruto na ghasia za uchaguzi wamejitoa katika kesi hiyo ambapo upande wa mashtaka umesema walitishiwa na kuhongwa ndoyo maana wakajitoa.
Kutokana na kujitoa kwao ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda ambaye ni mwendesha mashtaka wa Mahakama ya ICC
Aidha Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
Chanzo BBC


