
Rais Magufuli na viongozi wengine wa nchi za Afrika Mashariki
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Jijini Arusha, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema uamuzi huo umelenga kuhakikisha maslahi ya kila mwanachama yanalindwa.
“Tumeamua kuharisha mkutano wa leo kwa sababu mwanachama wetu mmoja Burundi hakuja kwa hiyo tumehairishwa mkutano hadi desemba 27 ili wote tuweze kuwepo katika kufanya maamuzi ya jumuiya,” amesema Rais Museveni.
Katika kikao hicho pia kililenga kujadili kuwa na shirikisho la kisiasa baina ya nchi wanachama pamoja na kujadili namna bora ya kufanya biashara, pamoja na kusoma ripoti ya kupendekeza Naibu Katibu wawili wa jumuiya hiyo.
Miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata pamoja wajumbe wengine wakiwemo Rwanda, Burundi, Sudan Kusini.